UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Peter Mikimba, kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
Ntibenda afanya uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhandisi huyo jijini hapa alipofanya kikao na Waandishi wa Habari na kusema Mhandisi Mikimba anakabiliwa na tuhuma za kushindwa kusimamia miradi ya ujenzi wa maabara, ujenzi na ukarabati wa barabara za wilaya.
Pia amesema ameshindwa kusimamia ujenzi wa nyumba za walimu kwa Mwaka wa Fedha 2013/14, ambapo athari zake zimejitokeza hivi karibuni katika miradi hiyo.
Aidha Ntibenda amemwagiza Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega kuunda Tume itakayochunguza tuhuma zinazomkabili Mhandisi Mikimba, kuanzia Mei 4 mwaka huu hadi Mei 15 na kuamuru kwa muda huo tume hiyo iwe imeshakamilisha uchunguzi wake.
Ametoa wito kwa watendaji wote wa serikali mkoani hapa, kusimamia kwa makini na weledi miradi yote inayotekelezwa na serikali kwa wananchi ili iwe na tija.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: