sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

JINSI YA KUEPUKA KUNUKA MDOMO


Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza
kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako. na ..........

Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.


Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

KINACHO SABABISHA HARUFU MBAYA MDOMONI
Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula). Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na madawa (medications) Kuvuta sigara, kunywa kahawa, ulaji wa vyakula vyenye viungo vikali kama vile vitunguu maji au thaumu.


NAMNA YA KUJUA KAMA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).


Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.


Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.
NAMNA YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA) 
Kula vyakula vyenye afya na vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri. Kusafisha meno mara kwa mara au kwa uchache mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, hii usaidia kuondoa au kujikinga na harufu mbaya mdomoni.


Vilevile unashauriwa kutumia KISAFISHA ULIMI (tongue cleaner) kusafishia ulimi wako. Tumia bazooka (chewing gum) ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka.

Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya. Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku. Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa au kila baada ya miezi sita kwa uchache.

Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.


NAMNA YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI!
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.


Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:

KUPIGA MSWAKI
Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.


Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.

KUNYWA MAJI MENGI
Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).


Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.

Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.

Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka (chewing gum) yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.

MWISHO: Hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.

KWA HABARI ZAIDI

JINSI YA KUTUNZA NGOZI YENYE MAFUTA


Sababu ya ngozi kuwa na mafuta hutokana na  na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango ambacho ambacho kinatakiwa. Lakini licha ya tezi hizo aina za sebaceous kuzalisha kiwango cha mafuta kwa wingi, zipo pia sababu nyingine ambazo zinafanya ngozi kuwa na mafuta ambazo

Kama ifuatavyo:

  • Kurithi.
  • Lishe.
  • Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini
  • Ujauzito.
  • Baadhi ya vipodozi .
  • Mabadiliko ya hali ya hewa hasa joto.

Na madhara ambayo yanatokana na ngozi yenye mafuta ni kwamba, ngozi huweza kutengeneza ngozi yenye tabaka lisiloisha vipele pamoja na  chunusi kwa muda mrefu.

Baada ya kuona baadhi ya sababu na athari ya ngozi kuwa mafuta,  sasa tuangalie namna ya kutunza ngozi zenye mafuta:

1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. Lakini Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au mara tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea kwa chunusi ambazo zitaufanya mwili kuwa na mafuta.

4. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.

5. Lakini pia unashauriwa ya kwamba hakikisha unatumia  mafuta ambayo  yametengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

Endapo utayazingatia hayo mwili wako utakwenda kuwa katika hali ya ubora zaidi, na kufurahia ngozi isiyo na kasoro.


KWA HABARI ZAIDI

MADHARA YA UNENE


Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata vifo.

Unene hupimwa kwa kutumia kipimo kinachotambulika kitaalamu kama BMI (yaani uzito kwa Kilogram kugawa kwa urefu kwa mita mara mbili).

Tatizo la unene uliopindukia huweza kusababisha mhusika kutengwa katika jamii, kubaguliwa, kudhihakiwa hata kunyanyapaliwa hivyo kuleta madhara kisaikologia kwa mgonjwa.

Sababu za unene uliopindukia ni pamoja kurithi. Mtoto aliyezaliwa na wazazi wanene,ana asilimia 80 ya kuwa mnene,aliyezaliwa na wazazi wembamba, ana asilimia 10 ya kuwa mnene.

Utamaduni na ukosefu wa nidhamu katika vyakula, pia unachangia unene uliopindukia.

Mfano; kuna ongezeko kubwa la watoto na vijana wanene kwa sasa mijini kuliko vijijini.

Madhara yaletwayo na unene uliopindukia ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na kulika kwa jointi hasa za miguu, maumivu kiunoni na katika nyonga, shinikizo la damu,kisukari, pia kukosa usingizi kutokana na kubanwa kwa hewa.

Mengine ni athma, kiungulia, mafuta mengi mwilini, magonjwa ya moyo na moyo kushidwa kufanya kazi na mawe katika kibofu cha nyongo.

Wagonjwa hujikuta wakishindwa kufanyakazi vyema ili kujipatia kipato, hivyo kuwa tegemezi, kunyanyapaliwa pia huleta matatizo ya kisaikologia kama nilivyoeleza awali.

Matibabu ya ugonjwa huu ni pamoja na kubadili mfumo na aina ya maisha. Hii ni pamoja na kuwa na nidhamu katika chakula na kufanya mazoezi.

Ni wazi kwamba wazazi na watoto wanaoishi mjini, wanakabiliwa na tatizo hili, kutokana na maisha ya mfumo mgando ( kula kazi bila jasho-kulala, au kula-kusoma-kulala).

Dawa pia zina patikana na zinasaidia kupunguza uzito walau kwa asilimia 10 kwa mwaka, lakini hufanyakazi vyema iwapo mfumo wa maisha utabadilishwa.

Matibabu ya muda mrefu ya tatizo hili na ambayo husaidia mgonjwa kwa kiwango kikubwa ni kufanyiwa upasuaji. Upasuaji katika tumbo ndiyo tiba mwafaka kwa unene uliopindukia.


KWA HABARI ZAIDI

JINSI YA KUZUIA CHUNUSI NA MABAKA USONI


Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.


Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .



Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.



Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.



Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.  



Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.



Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.



Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.

CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;



  1. UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
  2. VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
  3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
  4. DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
  5. MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
  6. MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
  7. JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
  8. FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
  9. HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
  10. USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
  11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi

DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana.

Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi

MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.

Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.

DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.

Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream, Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.

Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi.

Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.

DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.

Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na ”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”

Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.

MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.


MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.

Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi

MUHIMU
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
  1. Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
  2. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
  3. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
  4. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
  5. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
  6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
  7. Punguza mawazo
KWA HABARI ZAIDI

JINSI YA KUFANYA UWE NA UMBO DOGO

Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo.


Unalifahamu umbile la sifuri au saizi zero? 
Kwa wale wanaojali maumbo ya kupendeza saizi zero linatafsiriwa ni kuwa na kiuno kisichozidi inchi 23, nyonga 32 na kifua 31.  Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni mazoezi na ulaji wako, kwa kuwa mwangalifu katika kiasi cha kalori unachoingiza mwilini kila siku.

Unatakiwa kuwa mwadilifu katika uchaguaji wako wa chakula, haimaanishi ukae na njaa. Inawezekana ikawa ni vigumu kuelewa makala haya.



Kinachosisitizwa katika mpango huu, ni kuwa waangalifu katika upangiliaji wa vyakula. Aina hii ya mpangilio wa ulaji inafahamika zaidi kitaalamu kama ‘crash diet’ Kula kiasi cha kalori 400- 500 kwa siku. Lakini unatakiwa kufanya mazoezi angalau kwa saa mbili kwa siku, ili kupunguza mara mbili ya kiasi cha mafuta uliyokula katika siku hiyo.

Kunywa maji kwa wingi: 
Kwa kunywa kiasi kikubwa cha maji itakusaidia kurahisisha umeng’enyaji wa chakula mwilini. Ni vyema mwili wako ukawa na maji ya kutosha ikiwa umeingia kwenye mpango huu wa ulaji Kula mboga za kijani: Zina Vitamini, protini na virutubisho vingine kwa wingi ambavyo ni muhimu kwa afya. Kama ilivyoainisha awali, utaratibu huu hauhamasishi kukaa na njaa, bali kula vyakula vilivyo bora kiafya.



Kula vyakula visivyokobolewa.
Mara nyingi vyakula vya aina hii, huwa na virutubisho muhimu na vinavyohitajika katika ustawi wa mwili.



Punguza wanga katika mlo wako. 
Badala yake unaweza kula protini na kuingiza vyakula kama mayai na samaki kwenye mlo wako.


Epuka kula vyakula vya mtaani. 
Vyakula kama chips, mihogo ya kukaanga na jamii yake vinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzito wa mwili na pia hulifanya zoezi la umeng’enywaji wa chakula tumboni kuwa gumu.

Kula supu za mbogamboga;
Supu kama ya kabichi licha ya kujaza tumbo, husaidia katika kurahisisha mfumo wa umeng’enyaji chakula tumboni.

Kula saladi na matunda kwa wingi. 
Hii itasaidia kukuweka sawa kiafya.



Jizuie kula vyakula vyenye sukari nyingi na hata vile vya mtaani unavyohisi vinaweza kukwamisha mpango wako wa kupungua.


Lakini pamoja na yote jipe mazoezi ya kutosha kama kukimbia, kuruka kamba au mazoezi ya kupunguza tumbo na maziwa


KWA HABARI ZAIDI