UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale, Mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za mauaji ya mke wake pamoja na mtoto wao ambao walikutwa wameuawa kwa kuchinjwa shingoni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniveture Mushongi, mtuhumiwa huyo alikamatwa na mwenzake jana usiku maeneo ya Zinga wakati akijaribu kutoroka kufuatia taarifa zilizotolewa na wananchi wa eneo hilo.
Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa majira ya saa kumi na nusu jioni kwenye vichaka vya Kaole, Kanda ya Dunda Wilayani Bagamoyo, mtuhumiwa huyo akiwa na mwenzake Rajabu Juma mkazi wa Makongo waliwaua Oliver Erasto na Emannuel Frowin kwa kuwachinja shingoni kwa kutumia kisu.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mauaji hayo yalitokana na wivu wa mapenzi ambapo mume huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu aliejulikana kwa jina moja la Hamza mkazi wa Kawe Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ya Polisi imeeleza kuwa mume wa marehemu akiwa na rafiki yake alimlaghai mkewe waongozane pamoja wakiwa na mtoto wao kwenda kuangalia ujenzi wa nyumba yao eneo la Kaole Wilayani Bagamoyo lakini walipofika huko ndipo walipomchinja mke na mtoto.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Bagamoyo na itakabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: