UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
“Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ukusanyaji wa mapato umekuwa chini ya makadirio kwa sababu mbalimbali, Serikali ya Awamu ya Tano itaongeza nguvu katika upanuzi wa wigo wa kodi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,tutahakikisha kwamba kila mtu anayestahili kulipa kodi analipa kodi stahiki”.
Kauli ya Rais Magufuli wakati, akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma Novemba 20 mwaka jana (2015), ambapo leo jijini Dar es Salaam Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 1.03 ambayo ni sawa na asilimia 99.5 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.040 katika kipindi cha mwezi Aprili 2016.
Akizungumza na wanahabari katika ofisi za mamlaka hiyo kamishina mkuu TRA Alphayo Kidata amesema kwa kipindi cha miezi miwili iliyobaki TRA imeadhimia kukusanya zaidi ya shilingi Trilioni 1.4 ilikufikia na kuvuka leongo la mwaka 2015-2016.
Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada za mbalimbali za kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015-2016 licha ya ya kuwepo na changamoto mbalimbali.
TRA imetoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wa kodi na kichocheo cha ukusanyaji wa mapato kwa kudai risiti za EFDS pale wanaponunua bidhaa au kupatiwa huduma,kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu wale wote wanaojihusisha na biashara za magendo.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: