sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » WAANGALIAJI WA VIDEO ZA NGONO HUATHILIKA KTK MAHUSIANO KIMAPENZI SOMA ZAIDI


post-feature-image

Ungana na LINK CLASSIC katika kipengele cha 

KUHUSU MAISHA, LOVE STORY & SMS 



Mada yetu ni:- 
WAANGALIAJI WA VIDEO ZA NGONO HUATHILIKA KTK MAHUSIANO KIMAPENZI SOMA ZAIDI

Nilikuwa nasoma makala kwenye gazeti moja nikakutana na habari ya mtu huyu ambaye ameathirika na kitendo cha kutazama picha za ngono na tendo la kufanya punyeto tokea akiwa shule ya sekondari. Akaendelea kusema kwa sasa amekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitatu lakini tatizo hilo linaendelea ingawa mke wake hajui jambo hilo linavyomsumbua. Kinachotokea ni kwamba anapokuwa peke yake ndani ya nyumba peke yake huangalia picha hizo na kuanza kupiga punyeto, ingawa alidhani angeacha mara tu baada ya kuoa.



Athari alizopata kwa kuendekeza tabia hizo ni kukosa hamu kufanya tendo la ndoa na mkewe wakati mwingine hivyo kuna wakati anapata ugomvi na mkwewe akidhani kwamba anakwenda nje ya ndoa. Aliandika habari yake ili aweze kupatiwa msaada namna gani ya kuondokana na tatizo hilo. Kutokana na mtaalamu huyo ambaye anashauri watu ambao wameangukia kwenye tatizo hilo ni kwamba tabia hizo zinaweza kukuharibia ndoa yako kabisa kama uko miongoni wa waathirika.



Hakuna jambo ambalo unaweza kuliacha kirahisi kama umezoea kufanya kwa muda mrefu, kubadili tabia mbaya kunahitaji nguvu ya ziada kujitoa na wewe mwenyewe kutumia juhudi kubwa kuhakikisha unaacha kabisa.

Tabia ya kuangalia picha za ngono ni mbaya na inakubidi kuacha kabisa, ingawa kuna watu wanaiona kama si tatizo kama umeona inakuletea shinda kwenye ndoa ujue ni tatizo wala hakuna namna nyingine ambayo unaweza kutetea jambo hilo.

Si rahisi kuacha ila unahitaji kutumia muda mwingi ukiwa na mkeo vilevile kujadili jambo hilo kwa pamoja ili kupata msaada kutoka kwake. Vile vile unahitaji kuepuka kukaa peke yako bila kazi yoyote ya msingi ndani ya nyumba ili kufuta mawazo ya kufanya punyeto au kuangalia picha za ngono.

Jadili na mkeo ili muweze kupata suluhisho la kudumu, mjulishe kwamba umekuwa na shida hiyo ili kuokoa ndoa yako ingawa unahitaji lugha nzuri ya kuleta mada hiyo mezani. Mke anaweza kukusaidia kutatua suala hilo kihisia na kimwili na kwamba anahitaji kuwa na wewe kwa ukaribu zaidi ingawa juhudi kubwa inakubidi wewe mwenyewe kudhamiria kwa dhati kabisa kuondokana na tabia hiyo mbaya.

Watu wengi ni waathirika wa vitendo hivi ambavyo wengine waliingia kwa mkumbo hasa shule za boarding wakajikuta wanafanya kama sehemu ya maisha bila kujua madhara yake siku za usoni. Ni wakati umefika kwamba jamii na vijana kujua kila tabia mbaya ambayo unaiingiza kwenye maisha yako ni rahisi sana kuianza lakini kuiacha ni vigumu na itakugharimu sana. Unahitaji hekima ya kutosha kuanza kupambana na vitu ambayo havina tija kwenye maisha binafsi.


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini




TWITTER    

LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana
LINK CLASSIC 

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply