Uongozi wa Kampuni ya IVORI IRINGA (I. F. B) Unapenda kuutaarifu Umma Hususani Walaji, Wauzaji wa Jumla na Reja Reja kuwa kumekuwepo na bidhaa ya CHOCOLATE ambayo inatoka NJE YA NCHI ambayo imefananishwa jina la Nembo ya Bidhaa zetu za IVORI CHOCOLATE na hivyo kuwachanganya wateja wetu juu ya uwepo wa bidhaa yetu hiyo nakujiuliza maswali yafuatayo
1-Je Tumebadilisha Jina la Kampuni yetu?
2-Je Tumebadilisha Muonekano wa Bidhaa yetu ya CHOCOLATE?
3- Je Tumebadilisha Bei ya Chocolate za Ivori?
Kutokana na maswali hayo yaliyojitokeza kwa Wateja wetu, Kampuni Ya IVORI IRINGA Inapenda kuutaarifu Umma yafuatayo
1-Kampuni ya IVORI-Iringa haijafanya mabadiliko yeyote juu ya muonekano wa bidhaa zake, Gharama yake wala Nembo yake, haswa ya IVORI CHOCOLATE, Hivyo inawaomba wateja wake kuzingatia Yafuatayo
1-Kuhakikisha kila bidhaa unayonunua ya IVORI ina Nembo Halisi ya IVORI yenye Herufi I mwanzoni na herufi I mwishoni.
isomeke IVORI CHOCOLATE na Sio IVORY CHOCOLATE
2-Bidhaa zetu zote zinatengenezwa TANZANIA,Tunajivunia Uzalendo wetu na ndio maana bidhaa zetu zote ni MADE IN TANZANIA .
3-Hakikisha kila Chocolate yetu unayoinunua ina Rangi ya kahawia ndani ya pakiti yake ikiwa na Ladha tamu ya maziwa ikitegenezewa na COCOA Halisi inayolimwa na Wakulima Nchini TANZANIA
4-Rangi ya kifungashio chake ni ya Njano iliyochanganywa na Rangi ya Zambarau.
5-Gharama zetu Elekezi ni Shilingi 1000 kwa Gram 40 na Shilingi 500 kwa Gram 20 na hatuna ujazo unaozid gram 40.
KUWA MJANJA USIDANGANYIKE KUNUUNUA BIDHAA FEKI,NUNUA BIDHAA ORIJINO ZA IVORI IRINGA, EPUKA KUTAPELIWA.
ZINGATIA-Iwapo kuna utofauti wa Bidhaa unayoiona na kuitilia shaka Tafadhari usisite kuwasiliana nasi.
Imetolewa na
MKURUGENZI MKUU
I. F. B
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: