sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » TFDA YAFUNGA MACHINJIO YA TABORA

MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imeifunga machinjio ya nyama ya mjini Tabora kwa muda usiojulikana, baada ya kushindwa kutekeleza makubaliano ya kuondoa uchafu na kukarabati mifumo ya maji safi na maji taka ili kunusuru afya za walaji.

Kaimu Meneja wa mamlaka hiyo Kanda ya Magharibi, Dk Edgar Mahundi alisema wamefikia hatua hiyo baada ya uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na mambo mengine kushindwa kufanya usafi kama walivyoagiza siku saba zilizopita.

Alisema TFDA iliipa manispaa hiyo wiki moja iwe imekarabati mifumo ya maji safi na maji taka pamoja na kuondoa uchafu uliokuwa umerundikana katika maeneo ya machinjio hayo.

Dk Mahundi alibainisha kuwa uongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Tabora ulichokifanya ni kuweka bomba la maji na kupima afya za watumishi wa machinjio hiyo pasipo kufanya usafi wa eneo linalozunguka machinjio hiyo.

Aliyataja baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa ni pamoja na kuchimba shimo la maji taka, eneo la kutupia kinyesi cha ng’ombe baada ya kuchinjwa , ukarabati wa jengo la banda la kuhifadhia ngozi pamoja na jengo linalotumika kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa.

Aidha Dk Mahundi amebainisha kuwa mamlaka hiyo iliagiza ujengwe uzio wa machinjio hiyo ambao umechakaa ikiwa ni pamoja na kuweka lango kuu moja ili kuzuia wizi wa mifugo.


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

Whatsapp +255 652 989 873



PINTEREST  TWITTER    

LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply