MENEJA wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), mkoani Pwani, Martin Madulu, ametoa mwito kwa wananchi kufuata taratibu za kuunganishiwa umeme, badala ya kujiunganishia kwa kuwatumia vishoka.
Mwito huo ulitolewa baada ya watu wanaotuhumiwa kujiunganishia umeme bila kufuata utaratibu kukamatwa katika mtaa wa Kwamfipa wilayani hapa. Alisema, kubainika kwa watu hao waliokuwa wanaiba umeme kumefuatia taarifa za wananchi kuhusu watu wanaohujumu miundombinu ya umeme katika eneo hilo.
“Wezi hao walikuwa wamezichimbia nyaya za umeme chini ya barabara kusambaza katika baadhi ya maeneo ikiwemo maduka, mabanda ya kuoneshea video, hali ambao ni hatari kwa usalama wa watu na mali zao, pindi majanga ya moto unaosababishwa na hitilafu ya umeme yanapotokea,” alisema.
Ofisa Usalama wa shirika hilo, Henry Byarugaba alisema, Tanesco inapata hasara kwa kupoteza mapato yake kutokana na wizi unaofanywa kwenye miundombinu yake, pamoja na wasio waaminifu kujiunganishia umeme kinyemela.
Byarugaba aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojiunganishia umeme kinyume cha utaratibu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja
ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL
zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: