ZAIDI ya Sh milioni 320 zimetumika kulipia mishahara kwa wafanyakazi hewa wa serikali katika mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainika kutokana na uhakiki uliofanywa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuwataka wakuu wa mikoa kuwabainisha wafanyakazi hao.
Yalibainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alipotoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake kutokana na kumalizika uhakiki wa watumishi wa serikali mkoani hapa.
Alisema siku 15 zilizokuwa zimetolewa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanawabainisha na kuwaondoa wafanyakazi hewa, zimeonesha katika mkoa huo kuna wafanyakazi hewa 62 ambao wanapokea mishahara hewa kwa vipindi tofauti.
“Tumebaini watumishi 62 kwa mchanganuo huu, watumishi 33 hawapo kazini kabisa na 29 ni watoro kazini kwa kipindi kirefu. Wengine hadi kufikia miezi 40 na wamekuwa wakipokea mishahara kama kawaida,” alisema.
Alisema kugundulika kwa watumishi hao hewa ni sawa na asilimia 0.5 ya watumishi wote katika mkoa huo kwani hadi sasa una watumishi wapatao 13,174 huku akisisitiza ya kuwa Idara ya Elimu ndiyo iliyoongoza kuwa na watumishi hao.
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja
ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL
zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: