Baadhi ya Wafuasi wa Ukawa wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Madiwani na wabunge wa jiji la Dar mda mfupi baada ya kuahirishwa uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Madiwani na Wabunge wa Ukawa, Manase John Mjema akitoa taarifa yake mbele baada ya kuahirishwa uchaguzi huo.Hali ilivyoonekana nje ya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar, baada wanachama wa CCM kuondoka eneo hilo.Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika (mbele) akiwaeleza wafuasi wa Ukawa maazio yao juu ya Uchaguzi huo.Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika viwanja vya Karimjee Dar.Wafuasi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakitoka ndani ya Ukumbi wa Karimjee baada ya kumaliza kikao chao kifupi wakati ulipokuwa umeahirishwa.
Tangazo lenye zuio la mahakama la kuzuia uchaguzi huo kwa muda.
UCHAGUZI wa Meya jiji la Dar es Salaam, uliokuwa ufanyike leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, umeahirishwa tena mpaka itakapotangazwa siku nyingine.
Akitangaza kuahirisha uchaguzi huo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo Theresia Mbwambo amesema kuwa, sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo ni kutokana na baadhi ya watu kufungua kesi mahakamani kuzuia uchaguzi huo. Hivyo akasema sababu ni court injuction yaani pingamizi la mahakama.
Baadhi ya wabunge na madiwani kutoka vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamepinga vikali kuahirishwa mara kwa mara uchaguzi huo huku wakiahidi kwenda mahakamani Jumatatu ili kufungua kesi ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, amesema hawakubaliani na sababu zilizotajwa za kuahirisha uchaguzi huo na ksisitiza kuwa watakwenda mahakamani kupinga hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea
kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website
hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website
hii
Pia waweza kuwasilina nasi
au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: