sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » DONDOO 8 MUHIMU ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI


Ikiwa zimetia siku mbili tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku waumini wakiipokea siku ya tatu baada ya Magharibi kutimia, hivyo siku ya leo kupitia mtembezi.com tunakuletea Dondoo mbalimbali za kuzingatia kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani

A) Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa kubwa ya kuongeza kwa wingi thawabu zako kwani thawabu zake ni kubwa kuliko miezi mingine, Tumia fursa hii wala usiiharibu au kuipoteza kwa mambo yasiyokuwa na faida kwako.


B) Mwenyezi Mungu (Allah) wa Ramadhan ndiye huyo wa mwezi Shaaban na miezi mingine, Jitihada yako ya ibada isiwe katika Ramadhani tu bali iwe ni jitihada ya kuendelea katika miezi yote ya mwaka.

C) Inajuzu mwanamke muislamu kusali taraweeh jamaa nyuma ya imamu kwa sharti; asali mistari ya nyuma, avae mavazi ya kusitiri mwili wake wote bila ya kuonyesha viungo na asipake mafuta mazuri ya kunukia, Siku hizi zipo sehemu misikitini za kusalia wanawake, Mwanamke akisali nyumbani kwake ni bora lakini akitaka kuswali Taraweeh jama na imam msikitini basi hakatazwi.

D) Usitie mkazo na bidii kusali nawafil na sunna(ibada zisizo za lazima) kama vile Taraweeh halafu ukapuuza swala za faradh (lazima) na pia kuchelewa kwenda kuswali sala ya Alfajiri Jamaa.


E) Baadhi ya watu hudhania kuwa rakaa za sala ya Taraweeh zimeungana na zinaendelea. Wanaosali husimama baada ya rakaa ya pili kuingia ya tatu kwa kutoa takbira na huiacha Takbiratl Ihraam katika rakaa ya tatu pamoja na kuwa wametoa Salaam baada ya rakaa ya pili na hili ni kosa, Na iliyokuwa sawa ni baada ya kutoa Salaam katika rakaa ya pili unasimama kuingia rakaa ya tatu bila ya Takbir, Halafu unasoma Tawjeeh kisha unatoa Takbiratul Ihraam.

F) Baadhi ya watu husali swala ya Taraweeh mbio mbio ili wakamilishe rakaa ishirini, Ni bora kusali rakaa nane kwa utulivu kuliko kusali rakaa ishirini mbio mbio, Kwa sababu kusali kwa utulivu inakutia utulivu (khushuu) katika sala yako na utulivu ndio roho ya Swala.

G) Ikiwa muislamu atachanganya sala (ikiwa amesafiri), ya Maghrib na ishaa kwa kuzisali zote wakati wa Magharibi (Jamaa Taqdiim), inafaa kusali Salatil Taraweeh baada ya sala ya Magharibi na Ishaa.

H) Na mwisho, ndugu yangu muislamu, kumi la mwisho katika mwezi mtukufu wa ramadhani uko usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu moja. Usiku huo ni Laylatul Qadr, Kazania sana kufanya ibada na kumdhukuru Allah katika siku hizo kumi, Kumi la mwisho si wakati wakushughulika na kujitayarisha na siku kuu ya Eid. Utakuwa umeipoteza fursa kubwa sana ikiwa kama hutoshughulika na ibada.

Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply