sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA MKUTANO

wfanyakazi wizara ya fedha na mipango

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Wizara ya Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika  kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi hasa kwa wale wenye ulemavu kwa  kuwajengea miundombinu rafiki sehemu za kazi ili  kuongeza ufanisi kazini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa mikutano hazina.Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo.
“Wizara pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake” . Alisisitiza James
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa  bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Kwa upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.
Maadhimisho hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla katika maeneo yao ya kazi.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango
IMG_8383
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply