UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Meneja Mkuu wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching’andu amebainisha mwelekeo wa shirika hilo huku akiwaasa wafanyakazi wake kutoa huduma bora ili kubadilisha shirika hilo na kuwa shirika bora la usafirishaji kikanda.
Mhandisi Chinga’ndu amesema hayo wakati akiongea na wafanyakazi zaidi ya 500 wa Dar es Salaam, mnamo Alhamisi Juni 16 2016 mjini Dar es Salaam. Mhandisi Ching’andu alieleza kuwa anayo furaha kuwa sehemu ya watendaji wa TAZARA na angependa kuongoza wafanyakazi wanaolipwa vizuri, wanaofanya kazi katika mazingira salama na kwa ushindani ili kutoa nafasi mbali mbali kwa wafanyakazi kukua na kujifunza.
“Ndoto zangu ni kuona TAZARA yenye wafanyakazi wenye furana na wanaojivunia kufanya kazi na kampuni hii.Nataka TAZARA ielekeze nguvu zake kwenye huduma na kuheshimu wateja wetu ili kuchangia katika kukuza uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kulipa kodi na gawio kwa wanahisha wetu,” alisema.
Aidha, aliwasihi wafanyakazi kujituma na kumpa ushirikiano, kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuondoa uovu wote uliochangia kurudisha maendeleo ya mamlaka hiyo.
Katika mikutano tofauti , aliyohutubia wafanyakazi, Meneja Mkuu amekuwa akiwataka wafanyakazi kutamka kwa pamoja “TAZARA Moja, TAZARA Moja, TAZARA Moja,” ambapo alitaka kila mfanyakazi kujenga dhana hiyo ili kuboresha umoja na ushirikiano kwenye shirika hilo.
Mhandisi Bruno Ching’angu aliwasihi wafanyakazi kuacha dhana potofu ya kuomba msaada na kuanza kufanya kazi kwa kuwa mamlaka hiyo ina kila kitu kinachohitajika ili kuzalisha mapato.
Alieleza kuwa aliacha kazi iliyokuwa ikimlipa vizuri nchiini Afrika Kusini na kujiunga na TAZARA kwasababu alijua fika mamlaka hii ilihitaji mageuzi makubwa ili kuzalisha kipato zaidi , kitakachotosha kulipa mshahara kwa wafanya kazi, kulipa kodi na gawio kwa wanahisa.
“ Kampuni hii ina kila kinachohitajika ili kutengeneza mapato. Wachina walikuja na kujenga miundo mbinu na kutuachia tuitumie ila wengine waliishia kupoteza maisha yao.
Pia Meneja Mkuu alilalamika kuwa “walitupatia vifaa vya kuvulia samaki na kutufundisha namna ya kuvua samaki, ila walivyotuacha navyo sisi tukarudia hali ya awali, ambapo tulitupa vifaa hivyo na kuanza kuomba samaki.”
Pia aliongeza kamwe hatakuwa sehemu ya utamaduni wa ombamba na hatohitaji kuongozi ombaomba huku akishauri wafanyakazi wote kuacha kuomba vitini na kujikita katika kuzalisha zaidi ili kupata kipato chao.
Meneja Mkuu alieleza kuwa ni muhimu kutambua utendaji wa sasa wa TAZARA ulivyokuwa unakatisha tamaa waanzilishi wa TAZARA ambao walifanya kazi sana ili kuhakikisha kuwa kuna reli inayounganisha Zambia na nchi za Afrika Mashariki.
“Unaweza toa hoja ya muda wa malipo na viwango vyake ila iko wazi kuwa fedha nyingi zimewekezwa TAZARA kwa miaka mingi na serikali ya China, Tanzania na Zambia na hivyo kila mtu anategemea sisi kurudisha fadhila kwa kutoa huduma bora.
Wafanyakazi walimshukuru meneja mkuu kwa kuchangia mawazo yake na kuahidi kushirikiana nae bega kwa bega ambapo pia walishauri awashughulikie mameneja wazembe.
Wafanyakazi pia walitaka mawasiliano katika ngazi zote yaboreshwe.
Mhandisi Ching’andu ametimiza miezi miwili tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli TAZARA mwezi Aprili 2016.
Mpaka sasa, Mkurugenzi Mtendaji ameshatembelea miundo mbinu ya kutoka Dar es Salaam kwenda New Kapiri Mposhi ili kukutana na kuongea na wafanyakazi wa mamlaka hii ili kuwaelezea mahitaji na nia ya kuboresha na kubadilisha taswira ya shirika hili, ambapo mizigo iliyoshushwa kwa mwaka 1976 ilishuka kutoka tani milioni 1.2 mpaka tani 90,000 kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Tangu kushika madaraka hayo, Mhandisi.Ching’andu amerejesha nidhamu kwenye utendaji wa mamlaka hii, ambapo kwa sasa mizigo, inasajiliwa na kusafirishwa ndani ya muda mfupi. vilevile treni zinazobeba abiria zinatumia muda mfupi, kwakuwa ukosefu huo wa nidhamu ulisababisha wateja kupungua.
Meneja Mkuu wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching’andu akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA (Hawapo pichani)
Baadhi ya wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: