sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » WALIOKIMBIA KUCHINJWA TANGA WAVAMIWA WALIKOHAMIA

UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Wananchi hao wamekumbwa na majanga hayo katika kijiji cha Kros ambako wamepewa hifadhi na wenyeji.

Imedaiwa kuwa majira ya saa nane za usiku wa juzi nyumba waliyokuwa wamelala iligongwa milango na kwamba walipokaidi kufungua, wavamizi hao waliupiga kwa nguvu kwa lengo la kutaka kuivunja.

Mashuhuda walisimulia kuwa hali hiyo ilisababisha taharuki.

Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) walifika kuokoa jahazi baada ya kupigiwa simu na mmoja wa wakazi wa kijiji, hicho kwa lengo la kuomba msaada wakihofia kuchinjwa, imeelezwa.

Mmoja wa wananchi hao waliokimbia kuchinjwa, Mponile Mluafu aliliambia Nipashe jana kijijini hapo kuwa usiku wa kumkia juzi, kulitokea tafrani baada ya watu wasiofahamika kugonga nyumba walimohifadhiwa wageni hao na kulazimisha wafunguliwe.

Mluafu alisema tukio hilo lilizusha hofu kwa kuwa watuhao baada ya kugonga na kutofunguliwa mlango, walitumia nguvu kutaka kuuvunja lakini majirani waliosikia kishindo hicho walipiga simu kambi ya Jeshi iliyopo karibu na muda mfupi kikosi cha askari wa Jeshi kilifika.

“Hawa watu nadhani walisikia taarifa ya simu wakatokomea kusikojulikana, na hata wanajeshi walipofika hawakukuta mtu eneo hilo,” alisema Mluafu.

Mluafu alisema hali imekuwa tete kwa wageni hao kwa kuwa baada ya tukio hilo, wenyeji walikimbia nyumba hiyo na kuwaacha peke yao kwa kuhofia kuchinjwa.

Mluafu alisema hali imekuwa tete kwa wageni hao kwa kuwa baada ya tukio hilo, wenyeji walikimbia nyumba hiyo na kuwaacha peke yao kwa kuhofia kuchinjwa.
Akizungumzia katika makazi mapya, Maimuna Said alisema hali ni ngumu kwani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula, malazi na kwamba hata maisha yao kwa ujumla bado yapo hatarini.

Kunyeta Hossen aliiomba serikali kuwapa msaada wa vyakula na malazi ili waepukane na maradhi kama kipindupindu.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwaimu akiambatana na Mbunge wa Muheza, Adadi Rajab, Mbunge wa Handeni, Omari Kigoda na Mbunge wa Pangani, Jumaa Aweso walitembelea makazi ya waathirika hao wa mauaji jana ili kujionea hali halisi.

Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply