UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Tarehe 20/06/2016 Majira Ya Saa 07:30hrs Katika Msitu Wa Buhindi
Uliopo Kijiji Cha Majengo Kata Ya Irenza Tarafa Buchosa Wilaya Ya Sengerema
Mkoa Wa Mwanza, Mariam Mathias Miaka [35] Mkazi Wa Kijiji Cha Nyangalamila
Alikutwa Akiwa Amekufa Kifo Cha Mashaka Katika Msitu Tajwa Hapo Juu Huku
Uchunguzi Wa Awali Ukionyesha Mwili Wake Ukiwa Na Mikwaruzo Kwenye Bega La
Kulia Pamoja Na Shingo.
Aidha Inadaiwa Kuwa Marehemu Aliondoka Nyumbani Kwake
Siku Ya Ijumaa Ya Tarehe 17.06.2016 Majira Ya Asubuhi Na Kwenda Katika Msitu
Tajwa Hapo Juu Kutafuta Kuni Na Ndipo Mauti Yalipo Mkuta Huko, Hadi Tarehe
20.06.2016 Majira Ya Saa 07:30hrs Ambapo Mwili Wake Uliweza Kuokotwa Katika
Msitu Huo.
Jeshi La Polisi Linamshikilia Mume Wa Marehemu Aitwaye Ponyiwa
Jeremia Miaka [37], Mkazi Wa Nyangalamila Kwa Mahojiano Zaidi Dhidi Ya Tukio
Hilo Kwani Alishindwa Kutoa Taarifa Polisi Na Kwa Majirani Anaoishi Nao Kwa
Kipindi Chote Ambacho Mkewe Hakuonekana Nyumbani Kwake Hivyo Kupelekea Kutiliwa
Shaka Katika Tukio Hilo.
Chanzo Cha Kifo Hicho Bado Hakijajulikana, Jeshi La Polisi Bado
Linaendelea Na Uchunguzi Pamoja Na Upelelezi Kuhusiana Na Tukio Hilo, Mwili Wa
Marehemu Tayari Umefanyiwa Uchunguzi Na Daktari Na Kukabidhiwa Kwa Ndugu Wa
Marehemu Kwa Ajili Ya Mazishi
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa
Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wananchi Akiwataka Waongeze Ushirikiano Kwa
Jeshi La Polisi Wakati Wote Panapotokea Jambo Au Tatizo Wasisite Kutaarifu Ili
Kuwaza Kuzui Vifo Vinavyoweza Kuepukika.
Katika Tukio La Pili
Kwamba Tarehe 20.06.2016 Majira Ya Saa 13:20hrs Na Kuendelea
Katika Maeneo Mbalimbali Ya Wilaya Ya Ilemela Mkoani Mwanza, Askari Walifanya
Doria Pamoja Na Misako Katika Mitaa Mbalimbali Ya Wilaya Tajwa Hapo Juu Na
Kufanikiwa Kuwakata Watu Wa Nne Wakituhumiwa Kujihusisha Na Biashara Haramu Ya
Bhangi Pamoja Na Pombe Aina Ya Gongo Kitendo Ambacho Ni Uvunjwaji Wa Sheria Na
Taratibu Za Nchi
Watuhumiwa Waliokamatwa 1.Janeth Masole Miaka [30], Mkazi Wa
Kiseke Aliyekamatwa Akiwa Na Bhangi Misokoto 83, 2. Suzana Dotto Miaka [50],
Mkazi Wa Igombe Aliyekamtwa Akiwa Na Pombe Ya Gongo Lita 60, 3. Maduru Mathias
Miaka [35], Mkazi Wa Igombe Aliyekamatwa Akiwa Na Mtambo Mmoja Wa Kutengenezea
Pombe Ya Gongo Na, 4. Busheshe Faida Miaka [20], Pia Mkazi Wa Igombe
Aliyekamatwa Na Bhangi Misokoto Miwili Kitendo Ambacho Ni Kinyume Na Sheria Na
Taratibu Za Nchi.
Aidha Watuhumiwa Wote Wa Nne Wapo Chini Ya Ulinzi Wa Jeshi La
Polisi Huku Mahojiano Dhidi Ya Tuhuma Za Uhalifu Wanaojihusisha Nao
Yakiendelea, Pindi Uchunguzi Ukikamilika Watafikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma
Za Uhalifu Zinazo Wakabili.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa
Polisi Ahmed Msangi Anawataka Wananchi Waendelee Kutulia Lakini Wakiendelea
Kuto Ushirikiano Kwa Jeshi La Polsi Ili Liweze Kufanya Kazi Vizuri Na
Kutokomeza Uhalifu Wa Aina Zote Katika Mkoa Wa Mwanza.
Imesainiwa Na:
Sacp: Ahmed Msangi
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: