sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » SPIKA NDUGAI AENDELEA NA MATIBABU INDIA

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

AFYA ya Spika wa Bunge, Job Ndugai bado haijatengemaa na imeelezwa kuwa bado anaendelea na matibabu nchini India.

Ndugai alikwenda India wiki mbili zilizopita na hadi sasa hajarudi nchini kutokana na hali yake kuelezwa kuwa si ya kuridhisha.

Wakati anaondoka takribani wiki mbili zilizopitaa ilielezwa kuwa amekwenda India kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake, lakini ni muda mrefu hajarejea nchini.

Ndugai alikwenda India kwa mara ya kwanza mwezi Desemba mwaka jana.

Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah alisema hivi karibuni kuwa ni kweli Ndugai yuko nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

“Ni kweli Spika yupo nje, lakini alikwenda kwa ajili ya kufanya uchunguzi tu, siyo kwamba anaumwa sana, hapana ila hii ni mara ya pili kwenda kufanya uchunguzi huo.,” alisema Dk Kashilila.

Ndugai hajaonekana hadharani kwa muda mrefu, hata katika shughuli muhimu za kitaifa ambazo zimekuwa zikifanywa na Rais John Magufuli, hivyo kuacha maswali mengi kutoka kwa wananchi.

Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply