UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Mbunge wa Ubungo mh Said Kubenea amemuandikia barua katibu wa Bunge Dk Thomas Kishalilah akidai kutoridhika na uamuzi wa Naibu Spika mh Tulia Ackson kupeleka shauri lake la madai ya kutoa taarifa za uongo dhidi ya Waziri wa Ujenzi na Jeshi la kujenga taifa Dk Hussein Mwinyi kwenye kamati ya haki maadili na madaraka ya Bunge akisema kuwa utaratibu uliotumika kumfikisha katika kamati hiyo umekiuka kanuni.
Mhe Kubenea anatoa malalamiko hayo kwa Naibu Spika na Kamati ya haki maadili na madaraka ya Bunge katika shauri dhidi yake lililofikishwa na Naibu Spika Dk Tulia Ackson ambaye aliieleza kamati hiyo kuwa Mh Kubenea alitoa taarifa za uongo wakati Waziri mwinyi anajibu hoja za wabunge kuhusu wizara yake kwenye kikao cha tarehe 10 May mwaka huu.
Katika kikao hicho mbunge huyo alihoji mgongano wa maslahi kati Waziri,Wizara na mkandarasi Henan Guijo Industry ya Uchina ambayo ina kandarasi ya kujenga nyumba za Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na wakati huo huo imejenga nyumba yake eneo la Sea View jijini Dar es Salaam ambapo amebainisha kuwa licha ya kuwa na uhakika na taarifa hiyo lakini pia kanuni zilizotumika katika tuhuma dhidi yake zimekiukwa.
Katika maelezo hayo aliyoyatoa kwa waandishi wa habari mjini Dodoma mhe Kubenea pia ameishambulia kamati ya Bunge ya haki maadili na madaraka ya Bunge kuwa imeundwa kwa lengo la kupunguza nguvu ya upinzani bungeni.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: