UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Juhudi za Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) pamoja na Taasisi isiyo ya kiserikali inayowajengea uwezo wanawake katika siasa (Ulingo) kwa kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi za kukomesha mfumo dume, bado zinakwamishwa na baadhi ya viongozi wanaotaka kuendeleza ubabe unaolenga kuendeleza mfumo dume.
Leo hii Wabunge Wanawake kutoka Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamelazimika kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kutoa kauli ya udhalilishaji hapo jana kwa wabunge wanawake wa Chadema kwamba ili wapate Ubunge wa Viti Maalumu lazima waitwe‘babe’; kauli hizi za viongozi wenye dhamana ya wananchi zina tija gani kwa Taifa la Tanzania?
Hayo yanajiri baada ya kuwepo kwa mvutano mkali hapo jana baina ya wabunge wa chama tawala na upinzani kurushiana vijembe na matusi ndani ya ukumbi wa bunge hali iliyopelekea Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Mwikabwe Waitara kutolewa nje ya ukumbi huo baada ya kutofautiana na Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga.
Wabunge hao wanawake kutoka vyama mbalimbali vya upinzani wamesisitiza adhma yao ya kujitoa katika Chama cha Wabunge Wanawake kutokana na kutopewa ushirikiano na wabunge wenzao wa chama tawala kwa madai kwamba wanaunga mkono udhalilishaji wa wanawake bungeni kwani wakati hayo yakifanyika wao walikuwa wakipiga makofi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: