UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Dar es Salaam ni moja ya majiji yanayoiunda Tanzania ukiachana na Tanga, Mbeya, Arusha na Mwanza; majiji haya yanaongoza kwa fursa za kibiashara, pia changamoto za utaratibu wa kufanya biashara ni moja ya vikwazo katika majiji hayo.
Kwa upande wa Jiji la Dar es Salaam hususan Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kumekuwepo na changamoto ya maeneo maalum ya kufanyia biashara jambo ambalo limepelekea wafanyabishara wengi kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi ikiwemo barabara za magari yaendayo haraka na wapita njia.
Kwa kuzingatia hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Isaya Mnguruni amesema kuwa halmashauri imetenga maeneo maalum yenye huduma stahiki kwa wafanyabiashara hao zaidi ya 2961, ambapo maeneo yaliyotengwa ni pamoja na Tabata Muslim, Ukonga, Kivule, na Kigogo Fresh.
Mkurugezi huyo amesema maeneo hayo yaliyotengwa yanauwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 6000 na yana huduma zote stahiki huku akiongeza kuwa maeneo hayo yatawekewa vituo vya daladala ili yaweze kufikika kiurahisi.
Hivyo mkurugenzi huyo amesema kuwa mpaka itakapofika Mei 8 mwaka huu wafanyabiashara wote wanaofanya maeneo yasiyorasmi waondoke mara moja na kwenda maeneo watakayopangiwa na Ofisi ya Afisa Mipango Miji, huku akisisitiza kuwa watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: