UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Yanayoendelea nchini Marekani hivi sasa katika Chama cha Republican kuelekea Uchaguzi Mkuu hayana tofauti sana na kile kilichotokea katika Chama cha Allience For Democratic Change (ADC) wakati wa Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar.
Aliyekuwa Mgombea Urais wa ADC Zanzibar Hamad Rashid alipingwa na chama chake baada ya kufanya maamuzi ya kushiriki katika uchaguzi huo pasipo ridhaa ya chama kwa kile kilichodaiwa alifanya mambo kwa kujiamulia pasipo kupata baraka za viongozi wa juu wa chama.
Wakati Hamad Rashid alipokuwa akiendelea kutifuana na viongozi wenzake ndani ya chama hicho na kukataa kumuunga mkono katika mbio za kuwania Urais katika Uchaguzi wa Marudio Zanzibar uliopelekea Hamad kushindwa, huko Marekani Spika wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, Paul Ryan, ameibuka na kusema waziwazi kuwa hana utayari wa kumuunga mkono Mgombea Urais wa chama hicho Donald Trump.
Trump ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini humo anayetazamiwa kupeperusha bendera ya Chama cha Republican katika kinyang’anyiro cha Urais nchini Marekani huku akichuana vikali na Mgombea wa Chama cha Democratic Hillary Clinton, amekumbana na upinzani wa waziwazi ndani ya chama chake kwa kile kilichodaiwa kushindwa kuheshimu taratibu za chama chake.
Hata hivyo migogoro iliyotokea katika Chama cha ADC kule Zanzibar nakupelekea chama hicho kuanguka katika Uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu, upinzani ulioibuka dhidi ya Donald Trump ndani ya chama chake utamnusuru na kuibuka mshindi katika Kongamano Kuu la Kitaifa la Chama Julai mwaka huu?
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: