BEKI wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi ameibuka na kusema kuwa mipango yake kutaka kuondoa kwenye timu hiyo ipo palepale kwa kuwa hata yeye anawadai pesa nyingi Yanga na hajui atalipwa lini.
Mwinyi ameyasema hayo kufuatia dili lake la kutaka kujiunga na AFC Leopard likielekea kuyeyuka licha kuandika barua ya kuomba kuachwa baada ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwinyi alisema haoni sababu ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kumuachia kwa kuwa ameshawapa barua ya kuomba kuachwa licha ya kuwadai pesa nyingi za mishahara pamoja ada ya usajili.
“Kiukweli mipango yangu ya kuondoka bado ipo kwa sababu hata kule Kenya usajili unafungwa Januari 15 na kikubwa ni ile timu kuweze kufika hapa wamalizane ili niondoke zangu.
“Nadhani hapa wao wamekuwa wagumu kwa sababu ya mkataba wangu bado mrefu ila kama hawatotaka kuniruhusu itabidi wanilipe malimbikizo yangu maana nawadai pesa nyingi zikiwemo za ada ya usajili na sijui nitalipwa lini,” alisema Mwinyi.
Ikumbukwe, uongozi wa Yanga kupitia katibu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa umeweka wazi suala la mchezaji huyo watakuwa tayari kumuachia kuondoka iwapo AFC Leopard watafuata utaratibu wa kuwapelekea barua rasmi na siyo kutegemea simu.
jiunge na group la whatsapp kupata habari haraka bofya hapa
https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: