Rais John Magufuli (katikati) akiwa ameshikana mikono akiomba dua na mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” (wa pili kushoto) na wanaye Johnson Nguza “Papii Kocha” (wa pili kulia), Francis Nguza (wa kwanza kulia) na Michael Nguza (kushoto) walipofika Ikulu Dar leo, Januari 2, kumshukuru kwa msamaha aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia
“Babu Seya” na wanaye Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza walipofika Ikulu leo.
Familia ya mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanaye Johnson Nguza “Papii Kocha”Francis Nguza na Michael Nguza leo walikwenda Ikulu, Dar, kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha wake aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia.
Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wanamuziki hao, miongoni mwa watu zaidi ya 8,000 aliowasamahe siku ya uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9 mwaka jana, wakati akilihutubia taifa huko Dodoma.
jiunge na group la whatsapp kupata habari haraka bofya hapa
https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: