Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kufanyia mkutano wake mkuu wa kila mwaka ambao utashirikisha Mataifa 19 wanachama wa shirikisho hilo utakaofanyika feb. 22, 2018 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa FIFA Gianni Infantino ndiye ataongoza mkutano huo huku Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura na Sekretarieti ya FIFA pamoja na rais wa CAF, Ahmad Ahmad na Sekreterieti yake, ni miongoni mwa wageni wa ngazi ya juu watakaohudhuria.
Agenda kadhaa zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa Fedha za FIFA kwaajili ya maendeleo ya mchezo wa soka, changamoto za usajili wa wachezaji kwa kutumia mtandao yaani TRANSFER MATCHING SYSTEM na kalenda ya kimataifa ya FIFA.
Baadhi ya nchi zitakazoshiriki katika mkutano huo ni Bahran, Saudi Arabia, Palestina, Algeria, , Ivory Coast, Tunisia, Mali na Niger.
jiunge na group la whatsapp kupata habari haraka bofya hapa
https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: