sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » POLEPOLE AWAZUNGUMZIA VIONGOZI WA DINI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole.
KATIBU  wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema Askofu Zakaria Kakobe  na viongozi wengine wa dini  hawajazuiwa kuongea na kwamba wako huru kutoa maoni yao.
Polepole alisema hayo jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni  aliposema hakuna mtu ambaye ametishwa kwa kusema ukweli juu ya jambo fulani ambalo huenda lipo au linatokea Tanzania.
“Hakuna mtu amezuiliwa kuongea ukweli  Tanzania, hakuna mtu ametishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.  Anayesema kuna mtu kazuiwa kuzungumza atakuwa na matatizo,  ila nachofahamu ni kwamba mtu kuzungumza lugha ya matusi, kwa mujibu wa katiba yetu na sheria zetu ni makosa,” alisema Polepole
Polepole aliendelea kusisitiza kuwa viongozi hao wa dini wapo wazi na huru kusema chochote kile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest Rwegasira, ilitoa onyo na kuwataka viongozi wa jumuiya za kidini kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya siasa.

jiunge na group la whatsapp  kupata habari haraka bofya hapa
KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply