sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » TUWAFUTE MACHOZI WAZAZI WETU!

UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Kutokana na mchango wa wazazi katika kutoa ulinzi na malezi bora kwa watoto, Septemba 17, 2012, Umoja wa Mataifa (UN) ulitangaza kila mwaka, Juni Mosi wazazi duniani kote bila kuzingatia rangi, dini, tamaduni au utaifa kusherehekea Siku ya Wazazi Duniani, ingawa bado wazazi wakumbana na changamoto kadha wa kadha kutoka kwa watoto wao.

Hakuna kitu kinachosikitisha kama kuona watoto wanawadharau wazazi wao, bila kufahamu changamoto ambazo wanazopitia kwenye malezi tangu miaka sifuri hadi utu uzima, kwani mtoto wa kwa mama hakui lakini kwa watoto hii ni tofauti kwani wanaona wakiwa wakubwa wanatakiwa kuwa na maisha mengine mbali na wazazi wao.

Changamoto wanazopata wazazi kwa watoto wao:

Kunyanyapaliwa: kisaikolojia inasemekana mtoto wa kiume huwa na ukaribu sana na mama yake mzazi, lakini pale anapokua hali inakuwa tofauti kwani anakuwa na maisha mengine na ukaribu hasa pale anapopata mwenza wake na pengine mkewe ndio chanzo cha kuweka mipaka na kuona wazazi si lolote si chochote kwa kujiona naye ameweza kuwa mzazi kwa kigezo cha mke na watoto.

Kutopata ukaribu kwa watoto wao: Majukumu yanamfanya mtoto asiwe na muda wa kukaa na wazazi, hivyo basi inapelekea ubaridi kwa wazazi na kuhisi upweke na wasiofaa. Katika kuadhimisha siku ya wazazi ni vyema kuwa na mtazamo chanya juu ya hili kwa kukumbuka na ukaribu na wazazi wako kama wao walivyotenga muda kwa ajili yako.

Imani za kishirikina: Hakuna jambo baya hapa duniani hadi kesho kwa Mungu kama kumhisi na kumshutumu mama au baba yako kwa uchawi, ni kweli katika jamii kuna baadhi ya wazazi wakiwa wazee wanatabia ambazo unaweza ukadhani hazina busara kwa upeo wako unaweza kumfikiria kuwa ni kwa sababu ya ushirikina, ndugu hebu rudi nyuma na ufikiri ni mchawi wa kiasi gani asikudhuru ulivyokuwa kuwa huna akili ya utambuzi wa mambo, tuache jamani kuingiza majozi kwenye nyoyo za wazazi wetu.

Nani kama mama na nani kama baba, ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezimungu , kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuwajali na kuthamini mchango wao na sio kujionesha pale wanapotoweka duniani kutokana na utandawazi mnawaposti kwenye Whatsapp na Instagram wakati wenyewe hawapo kwenye ulimwengu huu.


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
 +255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"FOR MORE INFO PLEASE"

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply