sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » UMUHIMU WA MAZOEZI KWA MWANAMKE MJAMZITO.


UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake.


Mazoezi wakati wa ujauzito yanasaidia:

Kupata usingizi mzuri usiku.
Kuondoa stress
Kulegeza na kunyoosha misuli ya uzazi na kuitayarisha kwa kazi ya kujifungua
Kupunguza kichefu chefu(morning sickness)na kiungulia(heartburn)

KUMBUKA:
Wakati unafanya mazoezi hakikisha kuwa husikii maumivi yoyote na ukipatwa namaumivu hakikisha unaonana na daktari haraka iwezekanavyo. Kumbuka usilaliemgongo wakati wa kufanya mazoezi au usifanye mazoezi aina ya jogging(kukimbia) au kuruka ruka(bouncing) na hakikisha mdundo wa moyo(pulse) na temperature yako ya mwili ziko sawa. 

1. Kunywa maji mengi kuzuia dehydration na angalia balance yako iko sawa ili kuzuia kuanguka.
Kama ulikuwa unafanya mazoezi kabla ya ujauzito unaweza kuendelea na mazoezi yafuatayo:
2. Kuogelea: 
Uzuri wa zoezi hili ni kwamba halihitaji nguvu nyingi linasaidia kurelax na misuli yote ya mwili inafanya kazi. Unaweza kuogelea kwa dakika 20 hadi 35 lakini uchukue break pale utakapoona umechoka au kuishiwa na nguvu au pumzi. Kuogelea pia kunasaidia kupunguza maumivu yatokanayo na miguu kuvimba.

3. Kutembea: 
Ni zoezi zuri sana kwa mwanamke mjamzito. Zoezi hili linaweza kufanywa dakika 20 had 35 kwa siku. Zoezi hili linapunguza stress, linasaidia chakula kushuka vizuri na digestion. Pia linasaidia katika kuweka sawa uti wa mgongo. Tatizo la uti wa mgongo kutokunyooka linasababishwa na tumbo kuongezeka na kukosekana kwa balance kwenye mwili.

Hiki ni chanzo cha maumivu ya mgongo. Kumbuka kuchuka break na kupumzika pale utakaposikia uchovu.
4. Kucheza Muziki: 
Mama mja mzito anaweza kucheza mziki kama zoezi hasa hasa mziki wa belly dancing wa kunyonga kiuno na miziki aina ya salsa. Hii inasaidia katika kulainisha misuli ya uzazi tayari kwa kujifungua, kusaidia kujifungua kwa urahisi na kupona kwa haraka zaidi baada ya kujifungua, kupunguza michirizi ya tumbo(stretch marks) inayojitokeza kwa ajili ya ngozi ya tumbo kuvutwa, pia inasaidia confidence ya mwanamke kujiona bado ana mvuto, kuondoa stress, kusaidia na balance, kupunguza maumivu ya mgongo na kusaidia kunyoosha uti wa mgongo.
5. Pia unaweza kuendesha baiskeli ila uangalie balance usianguke na usiendeshe sehemu zenye msongamano wa watu au traffic ikiwezekana tumia baiskeli special za mazoezi ndani ya gym(stationary bikes). 


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki, bila kusahau kuwashirikisha rafiki zako kutembelea website hii. 


+255 (0) 652989873 whatsapp


Karibu sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 


"FOR MORE INFO PLEASE"

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply