sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » TAMU YA NDOA KWA VIJANA

UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Ndoa ni jambo la kheri ndio maana hata kwenye vitabu vya dini, bila kuchagua imani imesisitiza suala hili la ndoa kwani ni njia njema ya kuepuka mambo yasiyokuwa sahihi lakini pamoja na maandiko yanayoonesha umuhimu wa jambo hili bado vijana wengi wa kiume kuliona kama halina msingi kwa kisingizio cha kuwa bado wanakula ujana.

Kupitia tovuti pendwa ya thelinkclassic.blogspot.com, inakuonesha nini kimefanywa na watafiti na kugundua faida kadha wa kadha kwa mwanaume atakayeamua kuingia kwenye muunganiko huu wa ndoa.

Zifuatazo ni faida ambazo unaweza kushtuka kwani umezikosa weweKapera

Huongeza Kipato

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wanasayansi zinaonesha kuwa wanaume walio katika ndoa hupata akili zaidi ya kutafuta pesa na kuongeza kipato, kwa sababu ya majukumu ya kifamilia na kwa upande wa wanaume mabachela wanakuwa wanapenda sana kutafuta pesa za kutumia na sio za maendeleo ili waweze kula bata kama watoto wa mjini wanavyosema.

Afya njema

Kutokana na tafiti zinaonesha kuwa wanaume walio ndani ya ndoa, wanakuwa na afya kutokana na matunzo wanayopata kwa wake zao, kwani ukiwa ana mke utapikiwa vizuri , utafuliwa na kunyooshewa hivyo basi hili jambo linakwenda sambamba na kupata huduma ya tendo la ndoa ambalo linachagiza afya njema kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume wasio kwenye ndoa ambao wanatumia muda mrefu kutafuta wasichana ili kuweza kutimiza haja zao za kimwili na pili kuhusu vyakula wanakuwa hawana ratiba ya kula na hivyo kula chochote kinachopatikana kutokana na mazingira.

Kuishi kwa muda mrefu

Wanasayansi wanasema kuwa, ndoa huongeza miaka saba (7) ya kuishi kwa mtu hivyo basi inapelekea kupunguza hatari ya kupata magonjwa kama kiharusi, mshtuko wa moyo na pili huongeza maisha kwa wale walio na ugonjwa wa saratani.

Hizo ndo faida za ndoa kwako Mwanaume, lakini sio kwamba ukimbilie ndoa bila kujipanga kimaisha au kufanya chaguo sahihi kwani inaweza isiwe suluhisho bali ni changamoto kwako, kwani thelinkclassic.blogspot.com, inashauri ni vyema ukaangalia faida kwanza na hasara au changamoto zake badaye kuliko kuendeleza maisha ya kisela ambayo hayana faida kwenye maisha yako.


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
 +255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"FOR MORE INFO PLEASE"

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply