UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph
Semboja (aliyeketi kulia) na Makamu wa Rais wa Chuo cha
Utawala China Bw. Chen Li (aliyeketi kushoto) wakisaini hati za
makubaliano ya ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili mapema leo
jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo, Chuo cha Utawala
China kitatoa fursa kwa watumishi wa umma nchini Tanzania
kwenda kupokea mafunzo ya kiutawala nchini China, pamoja
maandalizi ya makongamano tofauti tofauti na utoaji wa
mihadhara
kuhusu utawala, maendeleo ya majiji na ‘Kufahamu zaidi China’
yatakayofanyika hapa nchini na China.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph
Semboja (kulia) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Utawala China
Bw. Chen Li (kushoto) wakibadilishana hati za makubaliano ya
ushirikiano baada ya kusaini hati hizo mapema leo jijini Dar es
Salaam zenye malengo ya kutoa mafunzo ya kiutawala kwa
watumishi wa umma nchini.
Ujumbe kutoka Chuo cha Utawala China na baadhi ya
wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi wakiendelea na mazungumzo
wakati wa tafrija fupi ya utiaji saini ya hati za makubaliano kati ya
Taasisi hizo mbili zenye malengo ya kuongeza ufanisi serikalini
kupitia mafunzo kwa watumishi wa umma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa akizungumza
wakati wa tafrija fupi ya kusaini hati za makubaliano kati ya
Taasisi ya Uongozi na Chuo cha Utawala China.
Makamu wa Rais wa Chuo cha Utawala China Bw. Chen Li
akizungumza wakati wa tafrija fupi ya kusaini hati za makubaliano
kati ya taasisi yake ya Chuo cha Utawala China na Taasisi ya
Uongozi.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: