UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Tanzania, Zambia pamoja na Jamhuri ya watu wa China zimeanza mazungumzo ya pamoja kwa lengo la kushirikiana kuimarisha sekta ya miundombinu hususan kufufua Reli inayounganisha Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kukuza biashara na uwekezaji.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, amesema lengo ni kuangalia changamoto zilizopo, ikiwemo za kisheria na kiutawala katika shirika hilo ili hatimaye liweze kufanya kazi kwa namna iliyokusudiwa.
Awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2 za bidhaa kwa mwaka, wakati sasa inasafirisha tani laki 2 kwa safari inayotumia hadi siku kumi na mbili kutoka Dar es Saalam hadi New Kapiri Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.
Balozi Kijazi amesema lengo ni kuifufua Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia, kwa kuangalia umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.
Awali Tanzania na Zambia zilikubaliana kuwekeza zaidi katika reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: