UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watu ‘kuflash’ simu kunakosababishwa na sababu kadha wa kadha; katika zama hizi za utandawazi vitendo vya watu kuporwa simu za mkononi vimeripotiwa kwa kiasi kikubwa na wengi wao waliona kuwa njia sahihi nikuziflash ili zitumiwe na mtu mwingine bila kujua kuwa ni kosa la jinai kutokana na sheria za mtandao.
Hayo yamebainika wakati zimesalia siku 37 pekee ili Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuzima simu zote ambazo hazijakidhi viwango huku Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy akisisitiza watu kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea simu zao kuzimwa ifikapo June mwaka huu kwa kuwa tayari zitakuwa zimetolewa ubora wake.
“Unapoflash simu lazima fundi atakubadilishia Software zilizokuwepo toka mwanzo alafu utakuwa umeharibu ubora wa kile alichotengeneza mwanzo hivyo kutokana na sheria za umiliki unakuwa umetenda kosa la jinai”. Alisema Mungy
Mamlaka ya Mawasiliano imetoa rai kwa wanaonunua simu za mkononi kwa wakati huu wa lala salama kuwa makini kwa kuangalia namba za IMEI kwa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanapunguza bei za simu feki.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: