UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Katika kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa umeme wa kutosha serikali imefanya mapitio ya ripoti ya kuendeleza nishati ya joto ardhi kwa lengo la kuongeza uzalishaji mwingine wa umeme ambao utasaidia kwa Watanzania kupata dira ya maendeleo na kuongeza maendeleo ya uchumi wa Taifa .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo amesema kuanzisha kwa umeme wa jotoardhi unaotokana na mwamba wenye joto unaochemsha maji yaliyoingia ardhini ambapo utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa umeme hapa nchini .
Aidha maeneo yaliyolengwa ni Manyara, Ngozi Ngorongoro, Kisaki Majimoto Mara na mengineyo ambapo mvuke wake ni msafi na hauna madhara yeyote ambayo huweza kutumika kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani , viwandani kilimo na dawa .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface Njombe amesema kuwa ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongeza maendeleo ya ya jotoardhi nchini ambapo kuzalisha megawaiti 200 ifikapo mwaka 2020 na mega waiti 500 ifikapo mwaka 2025 na 2033 itazalisha megaweti 800 .
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: