UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuna mambo mengine ukiyasikia ni kama ndoto vile, kauli aliyoitoa baada ya kusikia kuwa Jimbo la Segerea Jijini Dar es Salaam halina Zahanati.
Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu Ndugai amesema mambo mengine ukisikia ni kama ndoto au hadithi za kufikirika, baada ya kusikia Kata ya Vingunguti na Kipawa Jijini Dar es Salaam hazina Zahanati.
Hayo yamebainishwa na Wabunge wa Jimbo la Segerea, Bona Kalua pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia (Chadema), Anatropia Theonest katika maswali yao kwa Wizara ya TAMISEMI, ya kutaka kujua kwanini maeneo hayo yenye mkusanyiko wa watu hayana Zahanati.
Bona Kalua alizitaja Kata ambazo hazina Zahanati katika jimbo lake ni pamoja na Kata ya Vingunguti ambayo ina wakazi wengi na haina zahanati lakini pia Kata ya Kipawa, Minazi Mirefu, Kiwalani, Kisukulu na Kimanga hazina Zahanati wala Vituo vya Afya.
Katika majibu yake Naibu Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo, alikiri kuwepo changamoto hiyo katika jimbo hilo na kusema kuwa serikali inalifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kutafuta eneo kubwa ambalo litafaa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati pamoja na Vituo vya afya ili kuondoa tatizo hilo.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: