UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Serikali ya Rais John Pombe Magufuli imeendelea kufanya jitihada kuhakisha kuwa wale wote wahujumu uchumi kwenye sakata la sukari wanachukuliwa hatua za kisheria na kuzuia matukio ya aina hiyo ambapo imeripotiwa kuwa Serikali imekamata tani 4900 Maeneo ya Mbagara jijini Dar es Salaam, tani 154 Dodoma na 622 Morogoro.
Serikali imeendelea na jitihada hizo ambapo mkoani Mbeya imekamata kiwanda bubu cha kufungasha sukari,kikiwa kwenye makazi ya watu katika eneo la Soweto jijini Mbeya ambacho kinatuhumiwa kufungasha sukari katika mifuko midogo yenye ujazo wa kati ya nusu kilo na kilo moja na kisha sehemu ya sukari hiyo kuiuza nje ya nchi na nyingine kusambazwa mitaani na kuwauzia wananchi kwa bei kubwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Mbeya,Nyerembe Munasa Sabi akiongozana na askari wa Jeshi la Polisi ameingia mitaani kutekeleza agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli la kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha sukari, na ndipo akafanikiwa kubaini kiwanda bubu cha kufungasha sukari kinachodaiwa kufanya kazi hiyo kinyume cha sheria na ndipo akaingiwa na hofu kuwa huwenda kiwanda hicho kinafungasha sukari iliyokwisha muda wake na kuwauzia wananchi.
Baada ya kukamatwa,mmiliki wa kiwanda hicho ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa sukari jijini Mbeya, Bushir Sanga yakaibuka malumbano makali dhidi yake na Mkuu wa wilaya kuhusu aina na uhalali wa mifuko inamofungashiwa sukari hiyo.
Baada ya kujiridhisha kuwa mfanyabiashara huyo hana kibali cha kufungasha bidhaa hiyo kutoka kwenye viwanda vya sukari vya ndani ya nchi,Mkuu huyo wa Wilaya akaamuru mfanyabishara huyo akamatwe ili akatoe maelezo polisi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: