
UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA, kuwa serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwa ajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo.
Waziri Mpango amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa shilingi Bilioni 20.125, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa halali.
Alitolea mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi Milioni 600 badala ya shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma yakiwasilishwa kama madeni mapya.
Dokta Mpango amesema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yaona watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na kujiridhisha kuwa ni halali.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz
ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua
LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: