UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
WATOTO wengi wametajwa kutumia mitandao ya kijamii, kuangalia mambo ambayo ni kinyume na maadili, jambo ambalo wameaswa kuitumia kujifunza mambo yenye manufaa kwao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga alisema hayo wakati akifungua mkutano wa tatu wa kamati kuu ya Baraza la Watoto Tanzania.
Aidha Nkinga aliwataka watoto kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuacha kulalamikia haki bila kutimiza wajibu.
Alisema ushiriki wa watoto ni moja ya haki tano za msingi kwa watoto wote, bila kujali tofauti zao na serikali inalipa suala la ushiriki wa watoto umuhimu wa kipekee katika mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka Wizara hiyo, Magret Mussai alisema, mkutano huo wa Baraza la Watoto ni muhimu na utawasaidia watoto kuangalia mambo yao ikiwemo kuangalia mikakati wa taifa ya ushirikishwaji wa watoto katika mambo mbalimbali.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz
ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua
LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: