UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema idadi ya watumishi hewa katika wilaya hiyo, imeongezeka hadi kufikia 89 wakiwa wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja.
Aidha, Hapi amebaini uwepo wa watumishi vivuli 81 katika kada ya ualimu na hivyo kutoa siku saba kwa maofisa utumishi wa wilaya hiyo, kuhakiki watumishi vivuli ili kubaini idadi yao na hasara waliyosababisha.
Hapi aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, na kueleza kuwa awali wakati akiingia katika ofisi yake wiki iliyopita alikuta kuna watumishi hewa 34 waliokuwa wamesababisha hasara ya Sh milioni 512.
Alisema baada ya kufanya uhakiki zaidi walibainika watumishi hewa wengine 55 walioisababishia serikali hasara ya Sh milioni 619 na hivyo kufanya jumla ya hasara kuwa Sh 1,131,754,081.
“Bado uhakiki wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunamaliza hili tatizo la watumishi hewa katika wilaya ya Kinondoni, awali walikuwa 34 lakini sasa wameongezeka 55 na kufikia 89,” alisema Hapi.
Akifafanua kuhusu watumishi vivuli, Hapi alisema watumishi hao ni wale ambao walihamishwa bila kufuata taratibu na hivyo kuendelea kupokea mshahara wa kazi yake ya awali badala ya kazi yake mpya.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz
ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua
LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: