Ungana na LINK CLASSIC katika kipengele
cha
HOT NEWZ
topic ni
RC MAKONDA ATANGAZA MOTISHA YA MILIONI 15 KWA MWALIMU BORA DAR
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa zawadi ya fedha kwa mwalimu atakayefaulisha mwanafunzi katika somo lake la sayansi, lengo likiwa ni kutoa motisha kwa walimu.
Makonda aliyasema hayo wakati akizindua programu ya kuwasaidia wanafunzi waliotoka katika familia masikini iliyoandaliwa na shule za Feza.
Feza wametoa Sh milioni 37.5 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi 150 wanaotoka katika familia masikini.
Makonda alisema atatoa Sh milioni 15 kwa mwalimu wa sekondari atakayefaulisha mwanafunzi katika masomo ya Sayansi na Sh milioni 10 kwa mwalimu wa kidato cha pili atakayefaulisha mwanafunzi katika masomo ya sayansi na Sh milioni tano kwa mwalimu wa shule ya msingi atakayefaulisha mwanafunzi.
“Niseme sitaishia kwenye kutoa fedha pekee, mwalimu huyo na familia yake watachagua mbuga yoyote ya wanyama watakayoitaka na nitagharamia kila kitu, naamini kwa kufanya hivyo kutajenga motisha hata kwa walimu wengine kuongeza jitihada na kuhakikisha anafaulisha wanafunzi,” alisema Makonda.
Aidha, Makonda amewashukuru Feza kwa kuamua kuwasaidia wanafunzi hao na amewataka wazazi kuhakikisha wanasimamia vyema fedha hizo ili zifanye kazi iliyokusuduwa.
“Sitopenda kusikia mama ametumia fedha hizo tofauti na nyinyi wanafunzi muwalipe wafadhili hawa kwa kusoma kwa bidii, hakuna mtu atakubali kuendelea kutoa msaada kwa mtu ambaye haoneshi juhudi,” aliongeza Makonda.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shule hizo, Isa Otcu alisema shule hizo zimeamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli katika harakati zake za elimu bure.
Alisema programu hiyo itatoa kiasi cha Sh 250,000 kwa kila mwanafunzi na tayari wameshaweka kiasi cha Sh 100,000 katika akaunti za wanafunzi hao kuanzia Januari mpaka Aprili.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: