sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » MAGHEMBE APOKEA MSAADA WA NDEGE KUTOKA UJERUMANI


SERIKALI ya Ujerumani imetoa msaada wa ndege maalumu aina ya “Husky A-1C Aircraft” kwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Malisili na Utalii kusaidia katika doria za kupambana na ujangili katika Pori la Akiba la Selous.

Msaada huo wenye thamani ya Euro 200,000 sawa na Sh milioni 498.2 umekabidhiwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Dk Gerd Muller katika hafla fupi iliyofanyika Matambwe ndani ya Pori la Akiba la Selous.

Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani Dk. Gerd Muller (wa pili kushoto) akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ndege maalum aina ya Husky A-1C kwa ajili ya kufanya doria za kupambana na ujangili katika hifadhi ya Akiba ya Selous wakati wa hafla iliyofanyika kwenye hifadhi hiyo ya Selous mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Kapteni Bernard Shayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Uhifadhi la Kimataifa la FZS, Dk Christof Schenck  (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Martin Laibooki. (Picha na HamzaTemba, Wizara ya Maliasili na Utalii).

Hafla hiyo ilihudhuriwa na maofisa wa Ubalozi wa Ujerumani nchini wakiongozwa na Balozi Egon Konchanke, viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa ya FZS, WWF, GIZ na KFW.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Maghembe alisema ndege hiyo itasaidia jitihada za Serikali za kupambana na ujangili kwa kufanya doria katika anga ya Pori la Akiba la Selous na kusaidia kutoa taarifa za kiuhalifu pale itakapobainika na kuchukuliwa hatua stahiki za kukabiliana na uhalifu huo.

“Ndege hii tunayoshuhudia mapokezi yake leo ni ukombozi kwa wanyamapori katika Pori hili la Akiba la Selous kwani itasaidia na kuimarisha doria za kupambana na ujangili ndani na kuzunguka eneo zima la hifadhi,” alisema Profesa Maghembe.

LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

+255 (0) 652989873 whatsapp



TWITTER    

LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply