Ungana na
LINK CLASSIC
katika kipengele cha
HOT NEWZ
topic ni
JPM AWAKUMBUKA WAJAPANI 40 WALIOKUFA KWENYE TETEMEKO LA ARDHI
JPM AWAKUMBUKA WAJAPANI 40 WALIOKUFA KWENYE TETEMEKO LA ARDHI
Rais John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri Mkuu wa Japan Mheshimiwa Shinzo Abe kufuatia vifo vya watu zaidi ya 40 vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi lililokikumba kisiwa cha Kyushu kilichopo kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Tetemeko hilo la ardhi limetokea Alhamisi iliyopita tarehe 14 Aprili, 2016 na kurudia tena siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ambapo limesababisha maporomoko makubwa ya udongo yaliyoharibu na kufunika makazi ya watu na miundombinu ya usafirishaji na mawasiliano.
Katika salamu hizo zilizopitia kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaharu Yoshida, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo mbaya na amempa pole nyingi Waziri Mkuu wa Japan Mheshimiwa Shinzo Abe.
“Nakupa pole sana Mheshimiwa Waziri Mkuu Shinzo Abe, na kupitia kwako natoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo” Amesema Rais Magufuli.
Aidha, Dkt. Magufuli amewapa pole wote waliojeruhiwa wakati wa maporomoko ya udongo, na amewaombea wapone haraka ili waweze kuungana na wananchi wengine wa Japan katika shughuli za kila siku za ujenzi wa Taifa lao.
Pia amevitakia kila la heri vikosi vya uokoaji vinavyoendelea na kazi hiyo katika maeneo yote yaliyoathirika.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: