Ungana na
LINK CLASSIC
katika kipengele cha
HOT NEWZ
topic ni
JANUARY MAKAMBA: MIFUKO YA PLASTIKI NI MARUFUKU KUTUMIKA NCHINI
JANUARY MAKAMBA: MIFUKO YA PLASTIKI NI MARUFUKU KUTUMIKA NCHINI
SERIKALI imepiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, kuanzia Januari Mosi mwakani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM).
Mwalongo alitaka kujua lini Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira itakaa na wadau wa mazingira kujadili suala la uzalishaji na matumizi ya mifuko hiyo ambayo imekuwa ikiongoza kwa uchafuzi wa mazingira.
January alisema sasa wanaendelea kufanya majadiliano kuhusu suala hilo na kwamba Januari Mosi mwakani itakuwa mwisho wa uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.
Awali, akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Luhaga Mpina alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wenye viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizowekwa.
“Wadau wote, wazalishaji na viwanda wanatakiwa kuhakikisha wanazalisha mifuko inayoruhusiwa yenye unene usiopungua mikroni 50, tutachukua hatua kwa viwanda vitakavyokiuka ikiwemo kufunga viwanda hivyo,” alisema Mpina.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: