MKUU wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amemsweka rumande Mhandisi wa Ujenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Saimon Ngagani kutokana na kukaidi agizo lake la kumtaka kufanya maandalizi mapema ya kuchimbia mapipa ya kuweka taka nyepesi katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.
Akizungumza na baadhi ya wananchi katika stendi ya mabasi ya zamani wakati wa kuweka mapipa hayo, Matiro alisema shughuli ya uwekaji mapipa hayo ilikuwa ifanyike saa 1.30 asubuhi, lakini wamelazimika kufanya saa 3.30 asubuhi kutokana na uzembe wa mhandisi huyo.
Alisema mhandisi huyo alipewa kazi ya kuandaa kokoto na mchanga mapema, lakini matokeo yake hakufanya hivyo. Alisema mhandisi huyo licha ya kumwagiza yeye, lakini pia alimwagiza Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Lewis Kalinjuna kufanya maandalizi mapema ya vitu vinavyotakiwa kwenye kazi ya kuweka mapipa ya taka nyepesi, matokeo yake mpaka jana asubuhi hakuna kilichofanyika.
“Hakuna kokoto wala saruji eneo la kufanyia kazi, huu ni uzembe mkubwa, mkuu wa kituo uko wapi kamata huyu muweke ndani,”aliagiza mkuu huyo wa wilaya.
Pamoja na hatua hiyo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuyatumia mapipa hayo kwa kuweka taka nyepesi na waepuke kuweka taka ngumu.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: