Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja la Kigamboni litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu.
Amesema kazi inayoendelea sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja hilo ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.
Amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma ili lidumu kwa muda mrefu.“Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa Mbarawa.
Amebainisha kuwa Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wanapovuka katika daraja hilo.
Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalam wanaendelea na taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.
Amesema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.
Takribani shilingi bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na Kigamboni.
LINK CLASSIC: Asante
sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki
sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi
ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako
kutembelea website hii
pia waweza tupia namba yako ukawa unapata habari kupitia simu yako
bureeeeeeee...ila simu iwe smartphone
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp / Call - 0652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: