Kwenye zile kubwa ambazo zimenifikia leo March 17 ni pamoja na hii ya Rais wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuvutiwa na kipindi cha Clouds 360 chaClouds Tv mpaka akaamua kuwapigia simu moja kwa moja studio na kuwapongeza.
Kingine alichokisema Rais Magufuli ni kuwa yeye ni shabiki namba moja wa kipindi hicho na anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Clouds Media Group kama zoezi zima laMalkiaWaNguvu na mengine mengi.
Rais Magufuli ambaye wakati anapiga simu studio alikua na Mke wake Mama Janeth Magufuli,amewapongeza Watangazaji wa kipindi hicho Hudson Kamoga,Babie Kabae naSam Sasali,ambapo amepongeza namna ya uchambuaji wa Magazeti wa kipindi hicho.
Nimeinasa pia sauti ya Rais Magufuli akiongea live kwenye kipindi cha Clouds 360.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: