MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewagiza wakuu wa idara wa Halmashauri za jiji la Dar es Salaam kutoa ripoti za matatizo ya wananchi na jinsi walivyojipanga ndani ya masaa 24.
Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hizo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kuapishwa jana.
Makonda amesema wananchi wa Dar es Salaam wanakabiliwa na changamoto za ulinzi,maji,biashara pamoja na elimu hivyo lazima matatizo hayo yapate ufumbuzi katika kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hizo.
Makonda amesema kuwa kwa muda alioutoa wa masaa 24 ni mkubwa hivyo lazima wafanye kazi hiyo jinsi walivyojipanga katika kutatua changamoto hizo.
Amesema wakati umefika katika kuwatumikia wananchi kuwaondolea kero zao ambazo zinafanya kuwa na malalamiko yasioisha.
Makonda amesema amekutana na Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuzungumzanaye juu ya suala la ulinzi na usalama kwa wananchi.
Aidha amesema kuwa kukutana huko sio mara ya kwanza ataendelea ikiwa ni lengo la kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.
LINK CLASSIC: Asante
sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki
sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi
ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako
kutembelea website hii
pia waweza tupia namba yako ukawa unapata habari kupitia simu yako
bureeeeeeee...ila simu iwe smartphone
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp / Call - 0652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: