Rais John Magufuli, ameponda Mkataba wa Serikali na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, akisema wakati umefika nchi iachane na umeme wa wafanyabiashara na iwe na wake yenyewe.
Akiweka jiwe la msingi kwenye mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi II, Rais Magufuli alisema: “Ni lazima nchi yetu tuachane na umeme usio na uhakika, umeme wa kukodishakodisha, umeme wa kutumia watu na ndiyo maana kumekuwa na matatizo mengi mara IPTL, mara nini, ni kwa sababu tulizoea maumeme ya kukodisha kodisha, ya wafanyabiashara, kwa hiyo hatua hii ya umeme wetu, ambao tutaumiliki sisi wenyewe tutafanikiwa katika maendeleo
Tuachane na mitambo ya kukodi, tumechoka kufanyishwa biashara na wawekezaji, tunalipia `capacity charge’ za ajabu ajabu halafu tunalipia bei ya ajabu.
“Tunawapa shida Watanzania wa hali ya chini, kila mmoja anahitaji umeme, lakini wengine wanashindwa kuuvuta kwa sababu umeme ni wa juu.”
Katika kashfa ya Tegeta Escrow iliyosababisha kutafunwa kwa takribani Sh. bilioni 300, mbali na kung’oa baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, baadhi ya maazimio yaliyopitishwa na Bunge mpaka leo hakuna kilichofanyika.
Azimio la saba la Bunge lilisema kwa kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonyesha kuwa, Tanesco imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya shirika hilo, serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa shirika la umeme nchini kwa lengo la kuokoa fedha.
Agizo hilo lililotolewa mwishoni mwa mwaka 2014, lakini mpaka leo halijatekelezwa na inadaiwa kuwa kila mwezi Tanesco inailipa IPTL Sh. bilioni nane, izalishe ama isizalishe umeme.
Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyowasilisha ripoti yake Bunge la 10 juu ya Escrow, alisema: “Mapato ya nchi makubwa kuliko ya utumbuaji majipu yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya nchi na serikali inatazama Sh. bilioni nane zinalipwa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya Sh. bilioni 30 zimeshalipwa kwa IPTL/PAP.”
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: