Uvamizi wa majambazi kwenye Benki ya Access, Tawi la Mbagala Rangi Tatu wilayani Temeke jijini Dar, Ijumaa iliyopita umeibua mapya baada ya jambazi mmoja kukutwa na hirizi shingoni, Amani lina mlolongo wa mambo yote.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Mkoa wa Temeke, jambazi huyo aliyekutwa na hirizi ni yule aliyesimama na bunduki mbili barabarani akifyatua risasi juu ili kuzuia magari yanayotoka Posta na Kariakoo yasipite eneo hilo.
Free masonry (1)-001Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar,
Kamishna Simon Siro.
SIKIA SIMULIZI HII
“Hii kazi ngumu sana! Yule jambazi aliyeshika bunduki mbili na kusimama barabarani, tulipompiga risasi tulimkuta ana hirizi shingoni!
Lakini mbaya zaidi ni kwamba, ile hirizi ilikuwa kama inahema.
“Lakini cha ajabu sasa, baada ya kuonekana imetulia, yule jambazi naye akatulia, akawa ameshakata roho. Huu ujambazi wa kupewa ujasiri na hirizi naona unashika kasi. Majambazi wengi tukiwaua au kuwakamata tunawakuta na hirizi. Hirizi si kitu mbele ya risasi bwana,” alisema mtoa habari huyo.
Alisema hirizi hiyo nyeusi ilikuwa imeshonwa kwa uzi mnene na askari walipoiona, waliduwaa kwa vile jambazi huyo alionekana
kujiamini sana alipokuwa ameshika bunduki barabarani kiasi cha kuonekana tishio.
“Huenda hirizi ilimsaidia kwa namna moja au nyingine maana lazima alishanusurika wakati fulani nyuma kwa hiyo alijua ni ile hirizi.
Lakini pia yule bwana baada ya kupigwa risasi alionekana kubadilika rangi na kuwa mweusi sana,” alisema mnyetishaji huyo.
MAJAMBAZI WOTE WALIKUWA NA HIRIZI?
Simulizi nyingine kutoka kwa shuhuda mmoja wa tukio hilo ilisema kuwa, wakati majambazi hao wakianza kutimka kwa kutumia pikipiki zao, mmoja alisikika akiwasisitiza wenzake kuhakikisha hakuna anayevua hirizi wala kuruhusu ikatike.
“Nahisi wale majambazi wote walikuwa wana hirizi. Walipokuwa wakiondoka, mmoja alikuwa akiongea kama mchezaji uwanjani, akiwaambia wenzake kwamba wahakikishe hirizi zao hazikatiki wala hazidondoki,” kilisema chanzo hicho.
MADAI YA KISHIRIKINA
Kumekuwa na madai mbalimbali kutoka kwa polisi kwamba sehemu kubwa ya majambazi huenda kwa waganga wa kienyeji ‘sangoma’ kwa lengo la kujiganga kabla hawajaenda eneo la tukio kufanya ujambazi. Inasemekana kwamba waganga hao huwapa hirizi na kuwachanja chale kwa madai kwamba hawatauawa au risasi hazitaingia miilini mwao licha ya kwamba inapotokea hali ya kujibishana kwa risasi, polisi wamekuwa washindi mara zote.
RPC ATOA ONYO
Akizungumza na Amani juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ACP Andrew Satta aliwaonya watu kuachana na shughuli za ujambazi na kwenda kwa waganga kupewa hirizi kwani risasi haina cha hirizi.
Pia alisema jeshi lake limejiimarisha zaidi ili kupambana na uhalifu hivyo akawataka wahalifu wote kujisalimisha wenyewe polisi kabla hawajakutwa na mkono wa polisi ambao bado upo kuwasaka.
“Hayo mambo ya hirizi sijui nini! Mimi naona wanapoteza muda bure. Jeshi limejipanga vizuri, litawamaliza wote, kwani tuko mitaani kila kukicha,” alisema Kamanda Satta.
????????????????????????????????????
Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga
WAZIRI ANENA MAZITO
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga aliwataka majambazi wote kujisalimisha kwani kwa oparesheni iliyoanza kwa nchi nzima toka Ijumaa iliyopita, hakuna atakayesalimika.
VIGOGO WATAJWA KUHUSIKA
Wakati hali iko hivyo kwa jambazi huyo, kuna madai kwamba, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa nchini ‘vigogo’ ndiyo wamekuwa wakifadhili kwa pesa makundi ya kigaidi ili kusababisha mauaji katika jamii.
3Hilo limekuja baada ya tukio la Jumatatu iliyopita jijini Arusha ambapo, askari waliwaua watu watatu waliokutwa na silaha nzito za kivita ndani kama vile AK-47 (angalia picha ukurasa wa mbele) ambayo hutumika hata vitani.
Baadhi ya watu walioshuhudia mapigano ya askari polisi wa Arusha na watu hao, walishangaa kuona raia wanamiliki silaha za kivita mitaani.
“Haiwezekani watu wamiliki silaha za vitani hivihivi tu. Lazima baadhi ya matajiri wanatoa pesa nyingi kwa ajili ya kuviimarisha hivi vikundi nchini, iko siku moja huko mbele watafanya balaa zito,” alisema Fadhili Moreno, mkazi wa Njiro jijini Arusha.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea
kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website
hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website
hii
Pia waweza kuwasilina nasi
au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: