sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » ZITTO KABWE AFICHUA SIRI YA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

KIONGOZI mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe  amesema lengo la waliotaka kumwua mbunge Tundu  Lissu lilikuwa kuwanyamazisha wapinzani na kwamba majibu sahihi kwa mwaka 2018  ni kusema zaidi.Zitto Kabwe
Zitto ambaye pia ni mbunge wa kigoma mjini ametoa masimamo huo katika salam zake za mwaka mpya wa 2018, kupitia ukurasa wake wa facebook.Nawatakia heri ya mwaka mpya 2018. mwaka 2017ulikuwa changamoto lukuki lakini pia mafanikio makubwa kwetu kama chama. Mkutano wa miaka 50 ya Azimio la Arusha jijini Arusha ilikuwa mafanikio ya juu kiitikadi. Kwangu Mimi Hotuba ya Arusha ilikuwa bora kimaudhui na ilipaswa tutoe kitabu cha Hotuba ile
Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia Jijini Mwanza kuhusu Maendeleo bila kupoka Uhuru wa watu ulitusaidia kuweka msimamo wetu kuhusu ubinywaji wa haki na Uhuru unaoendelea nchini.
Tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia. 
Ilinigarimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani tukio lile. 
Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema zaidi.
Kuondoka wanachama waandamizi ilikuwa pigo. Pigo hili limetupa funzo kubwa sana na hivyo tutaendelea kuwepo na imara zaidi mwaka 2018.
Chama chetu kinawatakia heri ya mwaka 2018. Tunamshukuru Mungu kwa mwaka 2017
Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa chama cha Chdema alipigwa risasi mwezi Septemba mjini Dodoma alipokuwa akihidhuria vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa sasa hali ya Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki inaimarika kutoka na matibabu anayoyapata katika hospitali jijini Nairobi nchini Kenya.

jiunge na group la whatsapp  kupata habari haraka bofya hapa

https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF


KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply