Na mashirika ya kimataifa
MOTO mkubwa umeharibu takriban magari 1,400 kwenye jengo la ghorofa la kuegesha magari huko Liverpool nchini Uingereza na baadhi ya watu kulazimika kuukaribisha mwaka mpya kwenye makao ya mengine ya muda.
Baadhi ya magari kati ya 1400 yaliyoteketea kwa moto mapema hii leo.
Wazima moto wanasema moto huo uliotokea katika jengo la King's Dock karibu na ukumbi wa Liverpool Echo Arena, ni moto mbaya zaidi kuwahi kukabiliana nao
Polisi wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa moto kutoka kwa gari moja ulisambaa kwenda kwa mengine.
Watu walihamishwa kutoka katika majengo yaliyo karibu na jengo hilo kutokana na moshi.
Polisi wa Merseyside wamesema magari ya kuzima moto 21 yalikuwa eneo hilo na huku wazima moto wakisema kuwa wanachukua tahadhari ya jengo hilo kuporomoka.
Kwa mujibu wa polisi magari yote yaliyokuwa kwenye jengo hilo linaloweza kuegeshwa magari 1600 yaliharibiwa.
Wamewataka watu kubaki nyumbani na kufunga madirisha ikiwa wataona moshi kutoka kwa moto huo.
jiunge na group la whatsapp kupata habari haraka bofya hapa
https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA




No comments: