WAZIRI wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (CCM) amesema kuwa ukimpeleka mahakamani Askofu Zacharia Kakobe atashinda kwasababu watu wanasema inawezekana anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.
Kigwangalla aliyasema hayo jana Desemba 31, 2017 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo ameeleza kuwa ugonjwa unaotajwa kuwa huenda unamsumbua Kakobe dalili zake ni kujisifia.
Kigwangalla amefafanua aina ya ugonjwa huo wa akili ambao inawezekana unamsumbua Askofu Kakobe kuwa ni ‘Bipolar Disorder: Currently Mania’. Pia amesisitiza kuwa hata ukimpeleka mahakamani anaweza akashinda kwa kigezo hicho.
”Kuhangaika na mtu kama KAKOBE ni kupoteza muda bure. Kuna watu wanasema inawezekana akawa na ugonjwa wa akili ‘Bipolar Disorder: Currently Mania’ ambao katika dalili zake ni ‘delusions of grandeur’ . Akipelekwa mahakamani anaweza kutetewa kwa kigezo hiki na akashinda!” ameandika Kigwangalla.
jiunge na group la whatsapp kupata habari haraka bofya hapa
https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: