sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » NAIBU WAZIRI SHONZA ALIVYOPIGILIA MSUMARI KAULI YA RAIS


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema wizara yake haitasita kumchukulia hatua msanii yeyote ataekaidi  agizo la kuvaa mavazi yenye staha.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo katika uzinduzi wa Tamasha la Tanzania Tukuza Utalii Festival lenye  lengo la  kukuza utalii lililoandaliwa na Shirikisho la Waimbaji wa Nyimbo za Injili chini.

“Wasanii wote ambao wataendelea kukaidi agizo la  mheshimiwa Rais la kutokuvaa mavazi ya staha Wizara yangu haitawavumilia tutachukua hatua kwa yeyote bila kujali nafasi au umaarufu wake, kabla dhoruba haijawakumba wabadilike, kwenye kupiga rungu siangalii mtu usoni.,”amesema Naibu Waziri Shonza.

Siku chache zilizopita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli  wakati akihutubia Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM  alitoa tamko la kuwataka wasanii kuvaa mavazi ya heshima katika video za nyimbo zao.




jiunge na group la whatsapp  kupata habari haraka bofya hapa
KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply